Nenda kwenye maudhui

Maandishi yaleyale, viwango vinne

Mwanzo wa “Alice katika Nchi ya Ajabu” wa Lewis Carroll, uliotafsiriwa kutoka Kiingereza na mnyororo wetu, katika kila kiwango kati ya vinne. Kando yake, tafsiri ya rejea, iliyofanywa na kupitiwa kwa mkono.

Maandishi ya asili

Alice was beginning to get very tired of sitting by her sister on the bank, and of having nothing to do: once or twice she had peeped into the book her sister was reading, but it had no pictures or conversations in it, “and what is the use of a book,” thought Alice “without pictures or conversations?”

So she was considering in her own mind (as well as she could, for the hot day made her feel very sleepy and stupid), whether the pleasure of making a daisy-chain would be worth the trouble of getting up and picking the daisies, when suddenly a White Rabbit with pink eyes ran close by her.

There was nothing so very remarkable in that; nor did Alice think it so very much out of the way to hear the Rabbit say to itself, “Oh dear! Oh dear! I shall be late!” (when she thought it over afterwards, it occurred to her that she ought to have wondered at this, but at the time it all seemed quite natural); but when the Rabbit actually took a watch out of its waistcoat-pocket, and looked at it, and then hurried on, Alice started to her feet, for it flashed across her mind that she had never before seen a rabbit with either a waistcoat-pocket, or a watch to take out of it, and burning with curiosity, she ran across the field after it, and fortunately was just in time to see it pop down a large rabbit-hole under the hedge.

Lewis Carroll, Alice's Adventures in Wonderland (1865), sura ya I. Kazi ya umma.

Tafsiri ya rejea

Imefanywa na kupitiwa kwa mkono, bila tafsiri ya mashine.

Alice alikuwa ameanza kuchoshwa sana na kukaa kando ya dada yake ukingoni mwa mto, na kutokuwa na jambo lolote la kufanya: mara moja au mbili alikuwa amechungulia kitabu ambacho dada yake alikuwa akikisoma, lakini hakikuwa na picha wala mazungumzo ndani yake, “na kitabu kina faida gani,” aliwaza Alice, “kisicho na picha wala mazungumzo?”

Basi alikuwa akitafakari moyoni mwake (kadiri alivyoweza, kwani joto la siku ile lilimfanya ahisi usingizi mwingi na kuwa mzito wa akili) iwapo raha ya kusuka mkufu wa maua ya daisi ingestahili taabu ya kuinuka na kuchuma maua hayo, mara ghafla Sungura Mweupe mwenye macho ya rangi ya waridi akapita mbio karibu naye kabisa.

Hilo halikuwa jambo la kushangaza sana; wala Alice hakuona ni ajabu mno kumsikia Sungura akijisemea, “Ole wangu! Ole wangu! Nitachelewa!” (alipolitafakari baadaye, ilimjia akilini kwamba angepaswa kulistaajabia jambo hilo, lakini wakati ule yote yalionekana kuwa ya kawaida kabisa); lakini Sungura alipotoa kweli saa kutoka mfukoni mwa kizibao chake, akaitazama, kisha akaendelea na safari yake kwa haraka, Alice aliruka akasimama, kwa sababu wazo lilimpita akilini kama umeme kwamba hakuwahi kamwe kuona sungura mwenye mfuko wa kizibao, wala mwenye saa ya kutoa humo, na huku akiwaka kwa hamu ya kujua, alikimbia kuvuka shamba akimfuata, na kwa bahati nzuri aliwahi kumwona akitumbukia ndani ya shimo kubwa la sungura chini ya ua wa vichaka.

Msingi

mapitio mtambuka 1

Tafsiri za mashine za kifungu hiki zinaandaliwa.

Ubora

mapitio mtambuka 1

Tafsiri za mashine za kifungu hiki zinaandaliwa.

Premium

mapitio mtambuka 2

Tafsiri za mashine za kifungu hiki zinaandaliwa.

Umahiri

mapitio mtambuka 2

Tafsiri za mashine za kifungu hiki zinaandaliwa.

Mipangilio iliyotumika: uaminifu “Aminifu”, majina yamerekebishwa kwa lugha, uchapaji wa mazungumzo wa lugha lengwa.